Nahumu 3:11
Nahum 3:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wewe pia utalewa; utakwenda mafichoni na kutafuta kimbilio kutoka kwa adui.
Nahum 3:11 in English
Nahum 3:11 · Berean Standard Bible
You too will become drunk; you will go into hiding and seek refuge from the enemy.
Context
9Kushi* na Misri walikuwa nguvu zake zisizo na mpaka;
Putu na Libia walikuwa miongoni mwa wale walioungana naye. 10Hata hivyo alichukuliwa mateka
na kwenda uhamishoni.
Watoto wake wachanga walivunjwa vunjwa vipande
kwenye mwanzo wa kila barabara.
Kura zilipigwa kwa watu wake wenye heshima,
na watu wake wote wakuu walifungwa kwa minyororo. 11Wewe pia utalewa;
utakwenda mafichoni
na kutafuta kimbilio kutoka kwa adui. 12Ngome zako zote ni kama mitini
yenye matunda yake ya kwanza yaliyoiva;
wakati inapotikiswa,
tini huanguka kwenye kinywa chake alaye. 13Tazama vikosi vyako:
wote ni wanawake!
Malango ya nchi yako
yamekuwa wazi kwa adui zako;
moto umeteketeza mapingo yake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.