Native Bible

Nahum 1:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Shauri baya lolote wapangalo dhidi ya Bwana yeye atalikomesha; taabu haitatokea mara ya pili.

Nahum 1:9 in English

Nahum 1:9 · Berean Standard Bible

Whatever you plot against the LORD, He will bring to an end. Affliction will not rise up a second time.

Context

7Bwana ni Mwema, kimbilio wakati wa taabu. Huwatunza wale wanaomtegemea, 8lakini kwa mafuriko makubwa, ataangamiza Ninawi; atafuatilia adui zake hadi gizani. 9Shauri baya lolote wapangalo dhidi ya Bwana yeye atalikomesha; taabu haitatokea mara ya pili. 10Watasongwa katikati ya miiba na kulewa kwa mvinyo wao. Watateketezwa kama mabua makavu. 11Ee Ninawi, kutoka kwako amejitokeza mmoja, ambaye anapanga shauri baya dhidi ya Bwana na kushauri uovu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.