Native Bible

Nahum 1:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ee Ninawi, kutoka kwako amejitokeza mmoja, ambaye anapanga shauri baya dhidi ya Bwana na kushauri uovu.

Nahum 1:11 in English

Nahum 1:11 · Berean Standard Bible

From you, O Nineveh, comes forth a plotter of evil against the LORD, a counselor of wickedness.

Context

9Shauri baya lolote wapangalo dhidi ya Bwana yeye atalikomesha; taabu haitatokea mara ya pili. 10Watasongwa katikati ya miiba na kulewa kwa mvinyo wao. Watateketezwa kama mabua makavu. 11Ee Ninawi, kutoka kwako amejitokeza mmoja, ambaye anapanga shauri baya dhidi ya Bwana na kushauri uovu. 12Hili ndilo asemalo Bwana: “Ingawa wana muungano nao ni wengi sana, watakatiliwa mbali na kuangamia. Ingawa nimekutesa wewe, ee Yuda, sitakutesa tena. 13Sasa nitavunja nira zao kutoka shingo yako, nami nitazivunjilia mbali pingu zako.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.