Native Bible

Nahum 1:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Sasa nitavunja nira zao kutoka shingo yako, nami nitazivunjilia mbali pingu zako.”

Nahum 1:13 in English

Nahum 1:13 · Berean Standard Bible

For I will now break their yoke from your neck and tear away your shackles.”

Context

11Ee Ninawi, kutoka kwako amejitokeza mmoja, ambaye anapanga shauri baya dhidi ya Bwana na kushauri uovu. 12Hili ndilo asemalo Bwana: “Ingawa wana muungano nao ni wengi sana, watakatiliwa mbali na kuangamia. Ingawa nimekutesa wewe, ee Yuda, sitakutesa tena. 13Sasa nitavunja nira zao kutoka shingo yako, nami nitazivunjilia mbali pingu zako.” 14Hii ndiyo amri Bwana aliyoitoa kukuhusu wewe, Ninawi: “Hutakuwa na wazao watakaoendeleza jina lako. Nitaharibu sanamu za kuchonga na sanamu za kuyeyusha ambazo zipo katika hekalu la miungu yenu. Nitaandaa kaburi lako, kwa maana wewe ni mwovu kabisa.” 15Tazama, huko juu milimani, miguu ya huyo mmoja aletaye habari njema, ambaye anatangaza amani! Ee Yuda, sherehekea sikukuu zako, nawe utimize nadhiri zako. Waovu hawatakuvamia tena; wataangamizwa kabisa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.