Nahumu 1:15
Nahum 1:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Tazama, huko juu milimani, miguu ya huyo mmoja aletaye habari njema, ambaye anatangaza amani! Ee Yuda, sherehekea sikukuu zako, nawe utimize nadhiri zako. Waovu hawatakuvamia tena; wataangamizwa kabisa.
Nahum 1:15 in English
Nahum 1:15 · Berean Standard Bible
Look to the mountains— the feet of one who brings good news, who proclaims peace! Celebrate your feasts, O Judah; fulfill your vows. For the wicked will never again march through you; they will be utterly cut off.
Context
13Sasa nitavunja nira zao kutoka shingo yako,
nami nitazivunjilia mbali pingu zako.” 14Hii ndiyo amri Bwana aliyoitoa kukuhusu wewe, Ninawi:
“Hutakuwa na wazao
watakaoendeleza jina lako.
Nitaharibu sanamu za kuchonga na sanamu za kuyeyusha
ambazo zipo katika hekalu la miungu yenu.
Nitaandaa kaburi lako,
kwa maana wewe ni mwovu kabisa.” 15Tazama, huko juu milimani,
miguu ya huyo mmoja aletaye habari njema,
ambaye anatangaza amani!
Ee Yuda, sherehekea sikukuu zako,
nawe utimize nadhiri zako.
Waovu hawatakuvamia tena;
wataangamizwa kabisa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.