Marko 6:7
Mark 6:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
(6) Kisha Yesu akawa anakwenda kutoka kijiji kimoja hadi kingine akifundisha. (7) Akawaita wale kumi na wawili, akawatuma wawili wawili, na kuwapa mamlaka kutoa pepo wachafu.
Mark 6:7 in English
Mark 6:7 · Berean Standard Bible
Then Jesus called the Twelve to Him and began to send them out two by two, giving them authority over unclean spirits.
Context
5Hakufanya miujiza yoyote huko isipokuwa kuweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache na kuwaponya. 6Naye akashangazwa sana kwa jinsi wasivyokuwa na imani. 7(6) Kisha Yesu akawa anakwenda kutoka kijiji kimoja hadi kingine akifundisha. (7) Akawaita wale kumi na wawili, akawatuma wawili wawili, na kuwapa mamlaka kutoa pepo wachafu. 8Akawaagiza akisema, “Msichukue chochote kwa ajili ya safari isipokuwa fimbo tu. Msichukue mkate, wala mkoba, wala fedha kwenye mikanda yenu. 9Vaeni viatu, lakini msivae nguo ya ziada.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.