Marko 6:5
Mark 6:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hakufanya miujiza yoyote huko isipokuwa kuweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache na kuwaponya.
Mark 6:5 in English
Mark 6:5 · Berean Standard Bible
So He could not perform any miracles there, except to lay His hands on a few of the sick and heal them.
Context
3Huyu si yule seremala, mwana wa Maria? Na ndugu zake si Yakobo, Yose,* Yuda na Simoni? Dada zake wote si tuko nao hapa kwetu?” Nao wakachukizwa sana kwa ajili yake, wakakataa kumwamini. 4Yesu akawaambia, “Nabii hakosi heshima isipokuwa katika mji wake mwenyewe, na miongoni mwa jamaa na ndugu zake, na nyumbani kwake.” 5Hakufanya miujiza yoyote huko isipokuwa kuweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache na kuwaponya. 6Naye akashangazwa sana kwa jinsi wasivyokuwa na imani. 7(6) Kisha Yesu akawa anakwenda kutoka kijiji kimoja hadi kingine akifundisha. (7) Akawaita wale kumi na wawili, akawatuma wawili wawili, na kuwapa mamlaka kutoa pepo wachafu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.