Marko 6:3
Mark 6:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Huyu si yule seremala, mwana wa Maria? Na ndugu zake si Yakobo, Yose,* Yuda na Simoni? Dada zake wote si tuko nao hapa kwetu?” Nao wakachukizwa sana kwa ajili yake, wakakataa kumwamini.
Mark 6:3 in English
Mark 6:3 · Berean Standard Bible
Isn’t this the carpenter, the son of Mary and the brother of James, Joses,* Judas, and Simon? Aren’t His sisters here with us as well?” And they took offense at Him.
Context
1Yesu akaondoka huko na kwenda mji wa kwao, akiwa amefuatana na wanafunzi wake. 2Ilipofika siku ya Sabato, akaanza kufundisha katika sinagogi, na wengi waliomsikia wakashangaa.
Nao wakauliza, “Mtu huyu ameyapata wapi mambo haya yote? Tazama ni hekima ya namna gani hii aliyopewa? Tazama matendo ya miujiza ayafanyayo kwa mikono yake! 3Huyu si yule seremala, mwana wa Maria? Na ndugu zake si Yakobo, Yose,* Yuda na Simoni? Dada zake wote si tuko nao hapa kwetu?” Nao wakachukizwa sana kwa ajili yake, wakakataa kumwamini. 4Yesu akawaambia, “Nabii hakosi heshima isipokuwa katika mji wake mwenyewe, na miongoni mwa jamaa na ndugu zake, na nyumbani kwake.” 5Hakufanya miujiza yoyote huko isipokuwa kuweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache na kuwaponya.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.