Native Bible

Mark 6:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yesu akaondoka huko na kwenda mji wa kwao, akiwa amefuatana na wanafunzi wake.

Mark 6:1 in English

Mark 6:1 · Berean Standard Bible

Jesus went on from there and came to His hometown, accompanied by His disciples.

Context

1Yesu akaondoka huko na kwenda mji wa kwao, akiwa amefuatana na wanafunzi wake. 2Ilipofika siku ya Sabato, akaanza kufundisha katika sinagogi, na wengi waliomsikia wakashangaa. Nao wakauliza, “Mtu huyu ameyapata wapi mambo haya yote? Tazama ni hekima ya namna gani hii aliyopewa? Tazama matendo ya miujiza ayafanyayo kwa mikono yake! 3Huyu si yule seremala, mwana wa Maria? Na ndugu zake si Yakobo, Yose,* Yuda na Simoni? Dada zake wote si tuko nao hapa kwetu?” Nao wakachukizwa sana kwa ajili yake, wakakataa kumwamini.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.