Native Bible

Mark 4:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Pia akawaambia, “Ufalme wa Mungu unafanana na mtu apandaye mbegu shambani.

Mark 4:26 in English

Mark 4:26 · Berean Standard Bible

Jesus also said, “The kingdom of God is like a man who scatters seed on the ground.

Context

24Naye akawaambia, “Kuweni waangalifu na yale mnayosikia. Kipimo kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa ninyi, hata na zaidi. 25Kwa maana kila mtu aliye na kitu atapewa zaidi, naye atakuwa navyo tele. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyangʼanywa.” 26Pia akawaambia, “Ufalme wa Mungu unafanana na mtu apandaye mbegu shambani. 27Akiisha kuzipanda, usiku na mchana, akiwa amelala au ameamka, mbegu huota na kukua pasipo yeye kujua ikuavyo. 28Udongo huifanya iote kuwa mche, halafu suke, kisha nafaka kamili kwenye suke.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.