Native Bible

Mark 4:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Akiisha kuzipanda, usiku na mchana, akiwa amelala au ameamka, mbegu huota na kukua pasipo yeye kujua ikuavyo.

Mark 4:27 in English

Mark 4:27 · Berean Standard Bible

Night and day he sleeps and wakes, and the seed sprouts and grows, though he knows not how.

Context

25Kwa maana kila mtu aliye na kitu atapewa zaidi, naye atakuwa navyo tele. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyangʼanywa.” 26Pia akawaambia, “Ufalme wa Mungu unafanana na mtu apandaye mbegu shambani. 27Akiisha kuzipanda, usiku na mchana, akiwa amelala au ameamka, mbegu huota na kukua pasipo yeye kujua ikuavyo. 28Udongo huifanya iote kuwa mche, halafu suke, kisha nafaka kamili kwenye suke. 29Lakini nafaka inapokuwa imekomaa, mara mkulima huingia shambani na mundu wa kuvunia, maana mavuno yamekuwa tayari.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.