Marko 4:24
Mark 4:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Naye akawaambia, “Kuweni waangalifu na yale mnayosikia. Kipimo kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa ninyi, hata na zaidi.
Mark 4:24 in English
Mark 4:24 · Berean Standard Bible
He went on to say, “Pay attention to what you hear. With the measure you use, it will be measured to you, and even more will be added to you.
Context
22Kwa kuwa hakuna kilichofichika ambacho hakitafunuliwa, wala hakuna jambo lolote la siri ambalo halitaletwa nuruni. 23Mwenye masikio ya kusikia, na asikie.” 24Naye akawaambia, “Kuweni waangalifu na yale mnayosikia. Kipimo kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa ninyi, hata na zaidi. 25Kwa maana kila mtu aliye na kitu atapewa zaidi, naye atakuwa navyo tele. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyangʼanywa.” 26Pia akawaambia, “Ufalme wa Mungu unafanana na mtu apandaye mbegu shambani.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.