Native Bible

Mark 14:56 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wengi walitoa ushahidi wa uongo dhidi yake, lakini maelezo yao hayakukubaliana.

Mark 14:56 in English

Mark 14:56 · Berean Standard Bible

For many bore false witness against Jesus, but their testimony was inconsistent.

Context

54Petro akamfuata kwa mbali, hadi uani kwa kuhani mkuu. Huko akaketi pamoja na walinzi, akiota moto. 55Viongozi wa makuhani na Baraza la Wayahudi* lote wakatafuta ushahidi dhidi ya Yesu ili wapate kumuua. Lakini hawakupata jambo lolote. 56Wengi walitoa ushahidi wa uongo dhidi yake, lakini maelezo yao hayakukubaliana. 57Ndipo wengine wakasimama wakatoa ushahidi wa uongo dhidi yake, wakisema: 58“Sisi tulimsikia akisema, ‘Mimi nitalibomoa Hekalu hili lililojengwa na wanadamu, na katika siku tatu nitajenga jingine ambalo halikujengwa na wanadamu.’ ”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.