Native Bible

Mark 13:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wakati huo mtu yeyote akiwaambia, ‘Tazama, Kristo* huyu hapa!’ au, ‘Tazama, yuko kule,’ msisadiki.

Mark 13:21 in English

Mark 13:21 · Berean Standard Bible

At that time if anyone says to you, ‘Look, here is the Christ!’ or ‘There He is!’ do not believe it.

Context

19Kwa maana siku hizo zitakuwa za dhiki kuu ambayo haijapata kuwako tangu mwanzo, hapo Mungu alipoumba ulimwengu, mpaka leo, na wala haitakuwako tena kamwe. 20Kama Bwana asingelifupisha siku hizo, kamwe asingeliokoka mtu yeyote. Lakini kwa ajili ya wateule, wale aliowachagua, amezifupisha siku hizo. 21Wakati huo mtu yeyote akiwaambia, ‘Tazama, Kristo* huyu hapa!’ au, ‘Tazama, yuko kule,’ msisadiki. 22Kwa maana watatokea makristo wa uongo na manabii wa uongo, nao watafanya ishara na maajabu ili kuwapotosha, ikiwezekana, hata wale wateule. 23Hivyo jihadharini. Nimekwisha kuwaambia mambo haya yote mapema kabla hayajatukia.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.