Marko 11:21
Mark 11:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Petro akakumbuka na kumwambia Yesu, “Rabi, tazama! Ule mtini ulioulaani umenyauka!”
Mark 11:21 in English
Mark 11:21 · Berean Standard Bible
Peter remembered it and said, “Look, Rabbi! The fig tree You cursed has withered.”
Context
19Ilipofika jioni, Yesu na wanafunzi wake wakatoka nje ya mji. 20Asubuhi yake walipokuwa wakipita, wakauona ule mtini umenyauka kutoka juu hadi kwenye mizizi yake. 21Petro akakumbuka na kumwambia Yesu, “Rabi, tazama! Ule mtini ulioulaani umenyauka!” 22Yesu akawajibu, “Mwaminini Mungu. 23Amin, nawaambia, mtu yeyote atakayeuambia mlima huu, ‘Ngʼoka ukatupwe baharini,’ wala asione shaka moyoni mwake, bali aamini kwamba hayo asemayo yametukia, atatimiziwa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.