Native Bible

Mark 11:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yesu akawajibu, “Mwaminini Mungu.

Mark 11:22 in English

Mark 11:22 · Berean Standard Bible

“Have faith in God,” Jesus said to them.

Context

20Asubuhi yake walipokuwa wakipita, wakauona ule mtini umenyauka kutoka juu hadi kwenye mizizi yake. 21Petro akakumbuka na kumwambia Yesu, “Rabi, tazama! Ule mtini ulioulaani umenyauka!” 22Yesu akawajibu, “Mwaminini Mungu. 23Amin, nawaambia, mtu yeyote atakayeuambia mlima huu, ‘Ngʼoka ukatupwe baharini,’ wala asione shaka moyoni mwake, bali aamini kwamba hayo asemayo yametukia, atatimiziwa. 24Kwa sababu hiyo nawaambia, yoyote mtakayoyaomba mkisali, aminini ya kwamba mmeyapokea, nayo yatakuwa yenu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.