Marko 11:19
Mark 11:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ilipofika jioni, Yesu na wanafunzi wake wakatoka nje ya mji.
Mark 11:19 in English
Mark 11:19 · Berean Standard Bible
And when evening came, Jesus and His disciples went * out of the city.
Context
17Naye alipokuwa akiwafundisha, akasema, “Je, haikuandikwa kuwa:
“ ‘Nyumba yangu itaitwa
nyumba ya sala kwa mataifa yote’?
Lakini ninyi mmeifanya kuwa ‘pango la wanyangʼanyi.’ ” 18Viongozi wa makuhani na walimu wa sheria wakapata habari hizi, nao wakaanza kutafuta njia ya kumuua, kwa kuwa walikuwa wakimwogopa, kwa sababu umati wote ulikuwa unashangazwa na mafundisho yake. 19Ilipofika jioni, Yesu na wanafunzi wake wakatoka nje ya mji. 20Asubuhi yake walipokuwa wakipita, wakauona ule mtini umenyauka kutoka juu hadi kwenye mizizi yake. 21Petro akakumbuka na kumwambia Yesu, “Rabi, tazama! Ule mtini ulioulaani umenyauka!”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.