Mathayo 9:21
Matthew 9:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
kwa maana alisema moyoni mwake, “Kama nikigusa tu vazi lake, nitaponywa.”
Matthew 9:21 in English
Matthew 9:21 · Berean Standard Bible
She said to herself, “If only I touch His cloak, I will be healed.”
Context
19Yesu akaondoka akafuatana naye, nao wanafunzi wake pia wakaandamana naye. 20Wakati huo huo, mwanamke mmoja, ambaye alikuwa na ugonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, akaja nyuma ya Yesu, akagusa upindo wa vazi lake, 21kwa maana alisema moyoni mwake, “Kama nikigusa tu vazi lake, nitaponywa.” 22Yesu akageuka, naye alipomwona akamwambia, “Binti, jipe moyo mkuu, imani yako imekuponya.” Naye yule mwanamke akapona kuanzia saa ile ile. 23Yesu alipofika nyumbani kwa yule kiongozi wa sinagogi na kuwaona waombolezaji wakipiga filimbi za maombolezo na watu wengi wakipiga kelele,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.