Mathayo 9:23
Matthew 9:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yesu alipofika nyumbani kwa yule kiongozi wa sinagogi na kuwaona waombolezaji wakipiga filimbi za maombolezo na watu wengi wakipiga kelele,
Matthew 9:23 in English
Matthew 9:23 · Berean Standard Bible
When Jesus entered the house of the synagogue leader, He saw the flute players and the noisy crowd.
Context
21kwa maana alisema moyoni mwake, “Kama nikigusa tu vazi lake, nitaponywa.” 22Yesu akageuka, naye alipomwona akamwambia, “Binti, jipe moyo mkuu, imani yako imekuponya.” Naye yule mwanamke akapona kuanzia saa ile ile. 23Yesu alipofika nyumbani kwa yule kiongozi wa sinagogi na kuwaona waombolezaji wakipiga filimbi za maombolezo na watu wengi wakipiga kelele, 24akawaambia, “Ondokeni! Kwa maana binti huyu hakufa, bali amelala.” Wakamcheka kwa dhihaka. 25Lakini watu walipokwisha kutolewa nje, akaingia mle ndani na kumshika yule binti mkono, naye akaamka.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.