Mathayo 9:20
Matthew 9:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakati huo huo, mwanamke mmoja, ambaye alikuwa na ugonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, akaja nyuma ya Yesu, akagusa upindo wa vazi lake,
Matthew 9:20 in English
Matthew 9:20 · Berean Standard Bible
Suddenly a woman who had suffered from bleeding for twelve years came up behind Him and touched the fringe of His cloak.
Context
18Yesu alipokuwa akiwaambia mambo haya, mara akaingia kiongozi wa sinagogi akapiga magoti mbele yake, akamwambia, “Binti yangu amekufa sasa hivi. Lakini njoo uweke mkono wako juu yake, naye atakuwa hai.” 19Yesu akaondoka akafuatana naye, nao wanafunzi wake pia wakaandamana naye. 20Wakati huo huo, mwanamke mmoja, ambaye alikuwa na ugonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, akaja nyuma ya Yesu, akagusa upindo wa vazi lake, 21kwa maana alisema moyoni mwake, “Kama nikigusa tu vazi lake, nitaponywa.” 22Yesu akageuka, naye alipomwona akamwambia, “Binti, jipe moyo mkuu, imani yako imekuponya.” Naye yule mwanamke akapona kuanzia saa ile ile.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.