Mathayo 9:19
Matthew 9:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yesu akaondoka akafuatana naye, nao wanafunzi wake pia wakaandamana naye.
Matthew 9:19 in English
Matthew 9:19 · Berean Standard Bible
So Jesus got up and went with him, along with His disciples.
Context
17Wala watu hawaweki divai mpya kwenye viriba vikuukuu. Kama wakifanya hivyo, viriba vitapasuka nayo divai itamwagika, navyo viriba vitaharibika. Lakini divai mpya huwekwa kwenye viriba vipya, na hivyo divai na viriba huwa salama.” 18Yesu alipokuwa akiwaambia mambo haya, mara akaingia kiongozi wa sinagogi akapiga magoti mbele yake, akamwambia, “Binti yangu amekufa sasa hivi. Lakini njoo uweke mkono wako juu yake, naye atakuwa hai.” 19Yesu akaondoka akafuatana naye, nao wanafunzi wake pia wakaandamana naye. 20Wakati huo huo, mwanamke mmoja, ambaye alikuwa na ugonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, akaja nyuma ya Yesu, akagusa upindo wa vazi lake, 21kwa maana alisema moyoni mwake, “Kama nikigusa tu vazi lake, nitaponywa.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.