Native Bible

Matthew 26:69 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wakati huu Petro alikuwa amekaa nje uani. Mtumishi mmoja wa kike akamjia na kumwambia, “Wewe pia ulikuwa pamoja na Yesu wa Galilaya.”

Matthew 26:69 in English

Matthew 26:69 · Berean Standard Bible

Meanwhile, Peter was sitting out in the courtyard, and a servant girl came up to him. “You also were with Jesus the Galilean,” she said.

Context

67Kisha wakamtemea mate usoni na wengine wakampiga ngumi. Wengine wakampiga makofi 68na kusema, “Tutabirie, wewe Kristo! Ni nani aliyekupiga?” 69Wakati huu Petro alikuwa amekaa nje uani. Mtumishi mmoja wa kike akamjia na kumwambia, “Wewe pia ulikuwa pamoja na Yesu wa Galilaya.” 70Lakini Petro akakana mbele yao wote akisema, “Sijui hilo usemalo.” 71Alipotoka nje kufika kwenye lango, mtumishi mwingine wa kike alimwona, akawaambia watu waliokuwepo, “Huyu mtu alikuwa pamoja na Yesu, Mnazareti.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.