Native Bible

Matthew 26:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lakini wakasema, “Isiwe wakati wa Sikukuu, kusitokee ghasia miongoni mwa watu.”

Matthew 26:5 in English

Matthew 26:5 · Berean Standard Bible

“But not during the feast,” they said, “or there may be a riot among the people.”

Context

3Basi viongozi wa makuhani na wazee wa watu wakakusanyika katika jumba la utawala la kuhani mkuu, jina lake Kayafa. 4Wakafanya shauri ili kumkamata Yesu kwa siri na kumuua. 5Lakini wakasema, “Isiwe wakati wa Sikukuu, kusitokee ghasia miongoni mwa watu.” 6Yesu alikuwa Bethania nyumbani mwa Simoni aliyekuwa na ukoma, 7naye mwanamke mmoja akamjia akiwa na chupa ya marhamu yenye manukato ya thamani kubwa; akayamimina kichwani mwa Yesu alipokuwa ameketi mezani kula chakula.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.