Native Bible

Matthew 21:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Asubuhi na mapema, Yesu alipokuwa akirudi mjini, alikuwa na njaa.

Matthew 21:18 in English

Matthew 21:18 · Berean Standard Bible

In the morning, as Jesus was returning to the city, He was hungry.

Context

16Wakamuuliza Yesu, “Je, unasikia hayo hawa wanayosema?” Akawajibu, “Naam; kwani hamkusoma, “ ‘Midomoni mwa watoto wachanga na wanyonyao umeamuru sifa’?” 17Akawaacha, akatoka nje ya mji, akaenda hadi Bethania, akalala huko. 18Asubuhi na mapema, Yesu alipokuwa akirudi mjini, alikuwa na njaa. 19Akauona mtini kando ya barabara, naye akaukaribia, lakini hakupata tunda lolote ila majani. Ndipo akauambia, “Wewe usizae matunda tena kamwe!” Papo hapo ule mtini ukanyauka. 20Wanafunzi wake walipoona jambo hili, wakashangaa, wakamuuliza, “Imekuwaje mtini huu kunyauka ghafula?”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.