Native Bible

Matthew 21:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wanafunzi wake walipoona jambo hili, wakashangaa, wakamuuliza, “Imekuwaje mtini huu kunyauka ghafula?”

Matthew 21:20 in English

Matthew 21:20 · Berean Standard Bible

When the disciples saw this, they marveled and asked, “How did the fig tree wither so quickly?”

Context

18Asubuhi na mapema, Yesu alipokuwa akirudi mjini, alikuwa na njaa. 19Akauona mtini kando ya barabara, naye akaukaribia, lakini hakupata tunda lolote ila majani. Ndipo akauambia, “Wewe usizae matunda tena kamwe!” Papo hapo ule mtini ukanyauka. 20Wanafunzi wake walipoona jambo hili, wakashangaa, wakamuuliza, “Imekuwaje mtini huu kunyauka ghafula?” 21Yesu akawajibu, “Amin, nawaambia, kama mkiwa na imani wala msiwe na shaka, si kwamba mtaweza kufanya tu yale yaliyofanyika kwa huu mtini, bali hata mkiuambia huu mlima, ‘Ngʼoka, ukatupwe baharini,’ litafanyika. 22Yoyote mtakayoyaomba mkisali na mkiamini, mtayapokea.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.