Native Bible

Matthew 21:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Akawaacha, akatoka nje ya mji, akaenda hadi Bethania, akalala huko.

Matthew 21:17 in English

Matthew 21:17 · Berean Standard Bible

Then He left them and went out of the city to Bethany, where He spent the night.

Context

15Lakini viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walipoona mambo ya ajabu aliyofanya na kuwasikia watoto wakishangilia katika eneo la Hekalu wakisema, “Hosana Mwana wa Daudi,” walikasirika. 16Wakamuuliza Yesu, “Je, unasikia hayo hawa wanayosema?” Akawajibu, “Naam; kwani hamkusoma, “ ‘Midomoni mwa watoto wachanga na wanyonyao umeamuru sifa’?” 17Akawaacha, akatoka nje ya mji, akaenda hadi Bethania, akalala huko. 18Asubuhi na mapema, Yesu alipokuwa akirudi mjini, alikuwa na njaa. 19Akauona mtini kando ya barabara, naye akaukaribia, lakini hakupata tunda lolote ila majani. Ndipo akauambia, “Wewe usizae matunda tena kamwe!” Papo hapo ule mtini ukanyauka.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.