Native Bible

Matthew 18:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa kuwa alikuwa hawezi kulipa deni hilo, bwana wake akaamuru kwamba auzwe, yeye, mkewe, watoto wake na vyote alivyokuwa navyo, ili lile deni lipate kulipwa.

Matthew 18:25 in English

Matthew 18:25 · Berean Standard Bible

Since the man was unable to pay, the master ordered that he be sold to pay his debt, along with his wife and children and everything he owned.

Context

23“Kwa hiyo Ufalme wa Mbinguni unaweza kufananishwa na mfalme aliyetaka kufanya hesabu zake za fedha na watumishi wake. 24Alipoanza kufanya hesabu zake, mtu mmoja aliyekuwa anadaiwa talanta* 10,000, aliletwa kwake. 25Kwa kuwa alikuwa hawezi kulipa deni hilo, bwana wake akaamuru kwamba auzwe, yeye, mkewe, watoto wake na vyote alivyokuwa navyo, ili lile deni lipate kulipwa. 26“Yule mtumishi akampigia magoti, akamsihi yule bwana akisema, ‘Naomba univumilie, nami nitakulipa deni lako lote.’ 27Yule bwana wa huyo mtumishi akamwonea huruma, akafuta deni lake lote, akamwacha aende zake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.