Native Bible

Matthew 18:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Yule mtumishi akampigia magoti, akamsihi yule bwana akisema, ‘Naomba univumilie, nami nitakulipa deni lako lote.’

Matthew 18:26 in English

Matthew 18:26 · Berean Standard Bible

Then the servant fell on his knees before him. ‘Have patience with me,’ he begged, ‘and I will pay back everything.’

Context

24Alipoanza kufanya hesabu zake, mtu mmoja aliyekuwa anadaiwa talanta* 10,000, aliletwa kwake. 25Kwa kuwa alikuwa hawezi kulipa deni hilo, bwana wake akaamuru kwamba auzwe, yeye, mkewe, watoto wake na vyote alivyokuwa navyo, ili lile deni lipate kulipwa. 26“Yule mtumishi akampigia magoti, akamsihi yule bwana akisema, ‘Naomba univumilie, nami nitakulipa deni lako lote.’ 27Yule bwana wa huyo mtumishi akamwonea huruma, akafuta deni lake lote, akamwacha aende zake. 28“Lakini yule mtumishi alipokuwa anatoka nje, akakutana na mtumishi mwenzake aliyekuwa amemkopesha dinari* mia moja. Akamkamata, akamkaba koo akimwambia, ‘Nilipe kile ninachokudai!’

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.