Mathayo 17:6
Matthew 17:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wanafunzi waliposikia haya, wakaanguka chini kifudifudi, wakajawa na hofu.
Matthew 17:6 in English
Matthew 17:6 · Berean Standard Bible
When the disciples heard this, they fell facedown in terror.
Context
4Ndipo Petro akamwambia Yesu, “Bwana, ni vyema sisi tukae hapa. Ukitaka, nitafanya vibanda vitatu: kimoja chako, kingine cha Mose na kingine cha Eliya.” 5Petro alipokuwa angali ananena, ghafula wingu lililongʼaa likawafunika, na sauti ikatoka kwenye hilo wingu ikisema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa. Ninapendezwa naye sana. Msikieni yeye.” 6Wanafunzi waliposikia haya, wakaanguka chini kifudifudi, wakajawa na hofu. 7Lakini Yesu akaja na kuwagusa, akawaambia, “Inukeni na wala msiogope.” 8Walipoinua macho yao, hawakumwona mtu mwingine yeyote isipokuwa Yesu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.