Native Bible

Matthew 17:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Petro alipokuwa angali ananena, ghafula wingu lililongʼaa likawafunika, na sauti ikatoka kwenye hilo wingu ikisema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa. Ninapendezwa naye sana. Msikieni yeye.”

Matthew 17:5 in English

Matthew 17:5 · Berean Standard Bible

While Peter was still speaking, a bright cloud enveloped them, and a voice from the cloud said, “This is My beloved Son, in whom I am well pleased.* Listen to Him!”

Context

3Ghafula wakawatokea mbele yao Mose na Eliya, wakizungumza na Yesu. 4Ndipo Petro akamwambia Yesu, “Bwana, ni vyema sisi tukae hapa. Ukitaka, nitafanya vibanda vitatu: kimoja chako, kingine cha Mose na kingine cha Eliya.” 5Petro alipokuwa angali ananena, ghafula wingu lililongʼaa likawafunika, na sauti ikatoka kwenye hilo wingu ikisema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa. Ninapendezwa naye sana. Msikieni yeye.” 6Wanafunzi waliposikia haya, wakaanguka chini kifudifudi, wakajawa na hofu. 7Lakini Yesu akaja na kuwagusa, akawaambia, “Inukeni na wala msiogope.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.