Native Bible

Matthew 17:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lakini Yesu akaja na kuwagusa, akawaambia, “Inukeni na wala msiogope.”

Matthew 17:7 in English

Matthew 17:7 · Berean Standard Bible

Then Jesus came over and touched them. “Get up,” He said. “Do not be afraid.”

Context

5Petro alipokuwa angali ananena, ghafula wingu lililongʼaa likawafunika, na sauti ikatoka kwenye hilo wingu ikisema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa. Ninapendezwa naye sana. Msikieni yeye.” 6Wanafunzi waliposikia haya, wakaanguka chini kifudifudi, wakajawa na hofu. 7Lakini Yesu akaja na kuwagusa, akawaambia, “Inukeni na wala msiogope.” 8Walipoinua macho yao, hawakumwona mtu mwingine yeyote isipokuwa Yesu. 9Walipokuwa wakishuka kutoka mlimani, Yesu akawaagiza, “Msimwambie mtu yeyote mambo mliyoyaona hapa, mpaka Mwana wa Adamu atakapofufuliwa kutoka kwa wafu.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.