Mathayo 15:12
Matthew 15:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha wanafunzi wake wakamjia na kumuuliza, “Je, unajua kwamba Mafarisayo walichukizwa sana waliposikia yale uliyosema?”
Matthew 15:12 in English
Matthew 15:12 · Berean Standard Bible
Then the disciples came to Him and said, “Are You aware that the Pharisees were offended when they heard this?”
Context
10Yesu akaita ule umati wa watu, akawaambia, “Sikilizeni na mwelewe: 11kinachomfanya mtu kuwa najisi mbele za Mungu si kile kiingiacho kinywani mwake, bali ni kile kitokacho kinywani mwake.” 12Kisha wanafunzi wake wakamjia na kumuuliza, “Je, unajua kwamba Mafarisayo walichukizwa sana waliposikia yale uliyosema?” 13Akawajibu, “Kila pando ambalo Baba yangu wa mbinguni hakulipanda, litangʼolewa. 14Waacheni; wao ni viongozi vipofu, wanaoongoza vipofu. Kama kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, wote wawili watatumbukia shimoni.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.