Native Bible

Matthew 12:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Watu wote wakashangaa na kusema, “Je, yawezekana huyu ndiye Mwana wa Daudi?”

Matthew 12:23 in English

Matthew 12:23 · Berean Standard Bible

The crowds were astounded and asked, “Could this be the Son of David?”

Context

21Katika Jina lake mataifa wataweka tumaini lao.” 22Kisha wakamletea mtu aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu, na alikuwa kipofu na bubu. Yesu akamponya, hata akaweza kusema na kuona. 23Watu wote wakashangaa na kusema, “Je, yawezekana huyu ndiye Mwana wa Daudi?” 24Lakini Mafarisayo waliposikia jambo hili wakasema, “Mtu huyu anatoa pepo wachafu kwa uwezo wa Beelzebuli,* mkuu wa pepo wachafu.” 25Yesu alijua walichokuwa wakiwaza, hivyo akawaambia, “Kila ufalme ukigawanyika dhidi yake wenyewe huangamia. Hali kadhalika kila mji au watu wa nyumba moja waliogawanyika dhidi yao wenyewe hawawezi kusimama.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.