Native Bible

Matthew 12:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lakini Mafarisayo waliposikia jambo hili wakasema, “Mtu huyu anatoa pepo wachafu kwa uwezo wa Beelzebuli,* mkuu wa pepo wachafu.”

Matthew 12:24 in English

Matthew 12:24 · Berean Standard Bible

But when the Pharisees heard this, they said, “Only by Beelzebul,* the prince of demons, does this man drive out demons.”

Context

22Kisha wakamletea mtu aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu, na alikuwa kipofu na bubu. Yesu akamponya, hata akaweza kusema na kuona. 23Watu wote wakashangaa na kusema, “Je, yawezekana huyu ndiye Mwana wa Daudi?” 24Lakini Mafarisayo waliposikia jambo hili wakasema, “Mtu huyu anatoa pepo wachafu kwa uwezo wa Beelzebuli,* mkuu wa pepo wachafu.” 25Yesu alijua walichokuwa wakiwaza, hivyo akawaambia, “Kila ufalme ukigawanyika dhidi yake wenyewe huangamia. Hali kadhalika kila mji au watu wa nyumba moja waliogawanyika dhidi yao wenyewe hawawezi kusimama. 26Kama Shetani akimtoa Shetani, atakuwa amegawanyika yeye mwenyewe. Basi ufalme wake utawezaje kusimama?

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.