Luka 6:29
Luke 6:29 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kama mtu akikupiga shavu moja, mgeuzie na la pili pia. Mtu akikunyangʼanya koti lako, usimzuie kuchukua joho pia.
Luke 6:29 in English
Luke 6:29 · Berean Standard Bible
If someone strikes you on one cheek, turn to him the other also. And if someone takes your cloak, do not withhold your tunic as well.
Context
27“Lakini nawaambia ninyi mnaonisikia: Wapendeni adui zenu. Watendeeni mema wanaowachukia. 28Wabarikini wale wanaowalaani, waombeeni wale wanaowatendea mabaya. 29Kama mtu akikupiga shavu moja, mgeuzie na la pili pia. Mtu akikunyangʼanya koti lako, usimzuie kuchukua joho pia. 30Mpe kila akuombaye, na kama mtu akichukua mali yako usitake akurudishie. 31Watendeeni wengine kama ambavyo mngetaka wawatendee ninyi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.