Luka 3:12
Luke 3:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Watoza ushuru nao wakaja ili wabatizwe, wakamuuliza, “Bwana na sisi inatupasa tufanyeje?”
Luke 3:12 in English
Luke 3:12 · Berean Standard Bible
Even tax collectors came to be baptized. “Teacher,” they asked, “what should we do?”
Context
10Ule umati wa watu ukamuuliza, “Inatupasa tufanyeje basi?” 11Yohana akawaambia, “Aliye na kanzu mbili amgawie asiye nayo, naye aliye na chakula na afanye vivyo hivyo.” 12Watoza ushuru nao wakaja ili wabatizwe, wakamuuliza, “Bwana na sisi inatupasa tufanyeje?” 13Akawaambia, “Msichukue zaidi ya kiwango mlichopangiwa.” 14Askari nao wakamuuliza, “Je, nasi inatupasa tufanye nini?”
Akawaambia, “Msimdhulumu mtu wala msimshtaki mtu kwa uongo, bali mridhike na mishahara yenu.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.