Native Bible

Luke 23:32 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Watu wengine wawili wahalifu, walipelekwa pamoja na Yesu ili wakasulubiwe.

Luke 23:32 in English

Luke 23:32 · Berean Standard Bible

Two others, who were criminals, were also led away to be executed with Jesus.

Context

30Ndipo “ ‘wataiambia milima, “Tuangukieni!” na vilima, “Tufunikeni!” ’ 31Kwa maana kama wamefanya hivi kwa mti mbichi, kwa mti mkavu itakuwaje?” 32Watu wengine wawili wahalifu, walipelekwa pamoja na Yesu ili wakasulubiwe. 33Walipofika mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, hapo ndipo walipomsulubisha Yesu pamoja na hao wahalifu, mmoja upande wake wa kuume na mwingine upande wake wa kushoto. 34Yesu akasema, “Baba, wasamehe, kwa maana hawajui walitendalo!” Wakagawana nguo zake kwa kupiga kura.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.