Native Bible

Luke 23:33 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Walipofika mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, hapo ndipo walipomsulubisha Yesu pamoja na hao wahalifu, mmoja upande wake wa kuume na mwingine upande wake wa kushoto.

Luke 23:33 in English

Luke 23:33 · Berean Standard Bible

When they came to the place called The Skull,* they crucified Him there, along with the criminals, one on His right and the other on His left.

Context

31Kwa maana kama wamefanya hivi kwa mti mbichi, kwa mti mkavu itakuwaje?” 32Watu wengine wawili wahalifu, walipelekwa pamoja na Yesu ili wakasulubiwe. 33Walipofika mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, hapo ndipo walipomsulubisha Yesu pamoja na hao wahalifu, mmoja upande wake wa kuume na mwingine upande wake wa kushoto. 34Yesu akasema, “Baba, wasamehe, kwa maana hawajui walitendalo!” Wakagawana nguo zake kwa kupiga kura. 35Watu wakasimama hapo wakimwangalia, nao viongozi wa Wayahudi wakamdhihaki wakisema, “Aliokoa wengine! Ajiokoe mwenyewe basi, kama yeye ndiye Kristo wa Mungu, Mteule wake.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.