Walawi 24:3
Leviticus 24:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nje ya pazia la Ushuhuda ndani ya Hema la Kukutania, Aroni ataziwasha taa mbele za Bwana kuanzia jioni hadi asubuhi bila kuzima. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo.
Leviticus 24:3 in English
Leviticus 24:3 · Berean Standard Bible
Outside the veil of the Testimony * in the Tent of Meeting, Aaron is to tend the lamps continually before the LORD from evening until morning. This is to be a permanent statute for the generations to come.
Context
1Bwana akamwambia Mose, 2“Waagize Waisraeli wakuletee mafuta safi ya zeituni yaliyokamuliwa kwa ajili ya mwanga ili taa ziwe zinawaka daima. 3Nje ya pazia la Ushuhuda ndani ya Hema la Kukutania, Aroni ataziwasha taa mbele za Bwana kuanzia jioni hadi asubuhi bila kuzima. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo. 4Taa zilizo juu ya kinara cha dhahabu safi mbele za Bwana lazima zihudumiwe daima. 5“Chukua unga laini, uoke mikate kumi na miwili, ukitumia sehemu mbili za kumi za efa* za unga kwa kila mkate.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.