Walawi 24:5
Leviticus 24:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Chukua unga laini, uoke mikate kumi na miwili, ukitumia sehemu mbili za kumi za efa* za unga kwa kila mkate.
Leviticus 24:5 in English
Leviticus 24:5 · Berean Standard Bible
You are also to take fine flour and bake twelve loaves, using two-tenths of an ephah for each loaf,*
Context
3Nje ya pazia la Ushuhuda ndani ya Hema la Kukutania, Aroni ataziwasha taa mbele za Bwana kuanzia jioni hadi asubuhi bila kuzima. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo. 4Taa zilizo juu ya kinara cha dhahabu safi mbele za Bwana lazima zihudumiwe daima. 5“Chukua unga laini, uoke mikate kumi na miwili, ukitumia sehemu mbili za kumi za efa* za unga kwa kila mkate. 6Iweke katika mistari miwili, kila mstari mikate sita, uiweke mbele za Bwana juu ya meza iliyotengenezwa kwa dhahabu safi. 7Kando ya kila mstari, weka uvumba safi kama sehemu ya kumbukumbu ili kuwakilisha mikate kuwa sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa kuteketezwa kwa moto.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.