Native Bible

Leviticus 24:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Taa zilizo juu ya kinara cha dhahabu safi mbele za Bwana lazima zihudumiwe daima.

Leviticus 24:4 in English

Leviticus 24:4 · Berean Standard Bible

He shall tend the lamps on the pure gold lampstand before the LORD continually.

Context

2“Waagize Waisraeli wakuletee mafuta safi ya zeituni yaliyokamuliwa kwa ajili ya mwanga ili taa ziwe zinawaka daima. 3Nje ya pazia la Ushuhuda ndani ya Hema la Kukutania, Aroni ataziwasha taa mbele za Bwana kuanzia jioni hadi asubuhi bila kuzima. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo. 4Taa zilizo juu ya kinara cha dhahabu safi mbele za Bwana lazima zihudumiwe daima. 5“Chukua unga laini, uoke mikate kumi na miwili, ukitumia sehemu mbili za kumi za efa* za unga kwa kila mkate. 6Iweke katika mistari miwili, kila mstari mikate sita, uiweke mbele za Bwana juu ya meza iliyotengenezwa kwa dhahabu safi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.