Walawi 24:12
Leviticus 24:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nao wakamweka mahabusu mpaka mapenzi ya Bwana yawe wazi kwao.
Leviticus 24:12 in English
Leviticus 24:12 · Berean Standard Bible
They placed him in custody until the will of the LORD should be made clear to them.
Context
10Basi mwana wa mama Mwisraeli na baba Mmisri alikwenda miongoni mwa Waisraeli, nayo mapigano yakatokea ndani ya kambi kati yake na Mwisraeli. 11Huyu mwana wa mwanamke Mwisraeli akalikufuru Jina la Bwana kwa kulaani; kwa hiyo wakamleta kwa Mose. (Jina la mama yake aliitwa Shelomithi binti wa Dibri, wa kabila la Dani.) 12Nao wakamweka mahabusu mpaka mapenzi ya Bwana yawe wazi kwao. 13Ndipo Bwana akamwambia Mose: 14“Mchukue huyo aliyekufuru nje ya kambi. Wale wote waliomsikia akikufuru wataweka mikono juu ya kichwa chake, kisha kusanyiko lote litampiga mawe.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.