Walawi 24:13
Leviticus 24:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndipo Bwana akamwambia Mose:
Leviticus 24:13 in English
Leviticus 24:13 · Berean Standard Bible
Then the LORD said to Moses,
Context
11Huyu mwana wa mwanamke Mwisraeli akalikufuru Jina la Bwana kwa kulaani; kwa hiyo wakamleta kwa Mose. (Jina la mama yake aliitwa Shelomithi binti wa Dibri, wa kabila la Dani.) 12Nao wakamweka mahabusu mpaka mapenzi ya Bwana yawe wazi kwao. 13Ndipo Bwana akamwambia Mose: 14“Mchukue huyo aliyekufuru nje ya kambi. Wale wote waliomsikia akikufuru wataweka mikono juu ya kichwa chake, kisha kusanyiko lote litampiga mawe. 15Waambie Waisraeli: ‘Ikiwa mtu yeyote atamlaani Mungu wake, atakuwa na hatia kwa uovu wake;
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.