Native Bible

Joshua 19:48 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Miji hii na vijiji vyake ndio iliyokuwa urithi wa kabila la Dani, ukoo kwa ukoo.

Joshua 19:48 in English

Joshua 19:48 · Berean Standard Bible

This was the inheritance of the clans of the tribe of Dan, including these cities and their villages.

Context

46Me-Yarkoni na Rakoni, pamoja na eneo linalotazamana na Yafa. 47(Lakini Wadani walipata shida kulimiliki eneo lao; kwa hiyo walipanda kuishambulia Leshemu, wakaitwaa, wakawaua watu wake kwa upanga na kuukalia. Walikaa Leshemu na kuuita Dani kufuatana na jina la baba yao.) 48Miji hii na vijiji vyake ndio iliyokuwa urithi wa kabila la Dani, ukoo kwa ukoo. 49Walipomaliza kugawanya nchi katika migawo kulingana na sehemu zao zilizowaangukia, Waisraeli wakampa Yoshua mwana wa Nuni urithi katikati yao, 50kama vile Bwana alivyokuwa ameamuru. Walimpa mji alioutaka, ambao ni Timnath-Sera* ulio katika nchi ya vilima ya Efraimu. Naye akajenga mji, akakaa huko.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.