Native Bible

Joshua 19:49 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Walipomaliza kugawanya nchi katika migawo kulingana na sehemu zao zilizowaangukia, Waisraeli wakampa Yoshua mwana wa Nuni urithi katikati yao,

Joshua 19:49 in English

Joshua 19:49 · Berean Standard Bible

When they had finished distributing the land into its territories, the Israelites gave Joshua son of Nun an inheritance among them,

Context

47(Lakini Wadani walipata shida kulimiliki eneo lao; kwa hiyo walipanda kuishambulia Leshemu, wakaitwaa, wakawaua watu wake kwa upanga na kuukalia. Walikaa Leshemu na kuuita Dani kufuatana na jina la baba yao.) 48Miji hii na vijiji vyake ndio iliyokuwa urithi wa kabila la Dani, ukoo kwa ukoo. 49Walipomaliza kugawanya nchi katika migawo kulingana na sehemu zao zilizowaangukia, Waisraeli wakampa Yoshua mwana wa Nuni urithi katikati yao, 50kama vile Bwana alivyokuwa ameamuru. Walimpa mji alioutaka, ambao ni Timnath-Sera* ulio katika nchi ya vilima ya Efraimu. Naye akajenga mji, akakaa huko. 51Haya ndiyo maeneo ambayo kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa koo za kabila za Israeli waliyoyagawanya kwa kura huko Shilo mbele za Bwana penye ingilio la Hema la Kukutania. Hivyo wakamaliza kuigawanya nchi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.