Yoshua 10:14
Joshua 10:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Haijakuwepo siku nyingine kama hiyo kabla au baada, siku ambayo Bwana alimsikiliza mwanadamu. Hakika Bwana alikuwa akiwapigania Israeli.
Joshua 10:14 in English
Joshua 10:14 · Berean Standard Bible
There has been no day like it before or since, when the LORD listened to the voice of a man, because the LORD fought for Israel.
Context
12Katika siku ile ambayo Bwana aliwapeana Waamori kwa Israeli, Yoshua akanena na Bwana akiwa mbele ya Waisraeli akasema:
“Wewe jua, simama juu ya Gibeoni,
wewe mwezi, tulia juu ya Bonde la Aiyaloni.” 13Hivyo jua likasimama,
nao mwezi ukatulia,
hadi taifa hilo lilipokwisha
kujilipizia kisasi kwa adui wake,
kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Yashari.
Jua likasimama kimya katikati ya mbingu, likachelewa kuzama muda wa siku moja nzima. 14Haijakuwepo siku nyingine kama hiyo kabla au baada, siku ambayo Bwana alimsikiliza mwanadamu. Hakika Bwana alikuwa akiwapigania Israeli. 15Ndipo Yoshua akarudi kambini huko Gilgali pamoja na Israeli yote. 16Basi wale wafalme watano wakawa wamekimbia kujificha kwenye pango huko Makeda.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.