Yoshua 10:12
Joshua 10:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Katika siku ile ambayo Bwana aliwapeana Waamori kwa Israeli, Yoshua akanena na Bwana akiwa mbele ya Waisraeli akasema: “Wewe jua, simama juu ya Gibeoni, wewe mwezi, tulia juu ya Bonde la Aiyaloni.”
Joshua 10:12 in English
Joshua 10:12 · Berean Standard Bible
On the day that the LORD gave the Amorites over to the Israelites, Joshua spoke to the LORD in the presence of Israel: “O sun, stand still over Gibeon, O moon, over the Valley of Aijalon.”*
Context
10Bwana akawafadhaisha mbele ya Waisraeli, nao wakawashinda kwa ushindi mkuu huko Gibeoni. Israeli wakawafukuza kuelekea njia iendayo Beth-Horoni wakiwaua mpaka kufikia njia iendayo Azeka na Makeda. 11Walipokuwa wakikimbia mbele ya Israeli kwenye barabara iteremkayo kutoka Beth-Horoni hadi Azeka, Bwana akawavumishia mawe makubwa ya mvua kutoka mbinguni, na wengi wao wakauawa na hayo mawe kuliko wale waliouawa kwa upanga wa Waisraeli. 12Katika siku ile ambayo Bwana aliwapeana Waamori kwa Israeli, Yoshua akanena na Bwana akiwa mbele ya Waisraeli akasema:
“Wewe jua, simama juu ya Gibeoni,
wewe mwezi, tulia juu ya Bonde la Aiyaloni.” 13Hivyo jua likasimama,
nao mwezi ukatulia,
hadi taifa hilo lilipokwisha
kujilipizia kisasi kwa adui wake,
kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Yashari.
Jua likasimama kimya katikati ya mbingu, likachelewa kuzama muda wa siku moja nzima. 14Haijakuwepo siku nyingine kama hiyo kabla au baada, siku ambayo Bwana alimsikiliza mwanadamu. Hakika Bwana alikuwa akiwapigania Israeli.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.