Native Bible

Joel 3:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

nitayakusanya mataifa yote na kuyaleta katika Bonde la Yehoshafati* Hapo nitaingia kwenye hukumu dhidi yao kuhusu urithi wangu, watu wangu Israeli, kwa kuwa waliwatawanya watu wangu miongoni mwa mataifa na kuigawa nchi yangu.

Joel 3:2 in English

Joel 3:2 · Berean Standard Bible

I will gather all the nations and bring them down to the Valley of Jehoshaphat.* There I will enter into judgment against them concerning My people, My inheritance, Israel, whom they have scattered among the nations as they divided up My land.

Context

1“Katika siku hizo na wakati huo, nitakaporejesha neema ya Yuda na Yerusalemu, 2nitayakusanya mataifa yote na kuyaleta katika Bonde la Yehoshafati* Hapo nitaingia kwenye hukumu dhidi yao kuhusu urithi wangu, watu wangu Israeli, kwa kuwa waliwatawanya watu wangu miongoni mwa mataifa na kuigawa nchi yangu. 3Wanawapigia kura watu wangu na kuwauza wavulana ili kupata makahaba; waliwauza wasichana ili wapate kunywa mvinyo. 4“Sasa una nini dhidi yangu, ee Tiro na Sidoni, nanyi nchi zote za Ufilisti? Je, mnanilipiza kwa yale niliyoyafanya? Kama mnalipa, mimi nitalipiza juu ya vichwa vyenu kwa kasi na kwa haraka yale mliyoyatenda.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.