Yoeli 3:4
Joel 3:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Sasa una nini dhidi yangu, ee Tiro na Sidoni, nanyi nchi zote za Ufilisti? Je, mnanilipiza kwa yale niliyoyafanya? Kama mnalipa, mimi nitalipiza juu ya vichwa vyenu kwa kasi na kwa haraka yale mliyoyatenda.
Joel 3:4 in English
Joel 3:4 · Berean Standard Bible
Now what do you have against Me, O Tyre, Sidon, and all the regions of Philistia? Are you rendering against Me a recompense? If you retaliate against Me, I will swiftly and speedily return your recompense upon your heads.
Context
2nitayakusanya mataifa yote na kuyaleta
katika Bonde la Yehoshafati*
Hapo nitaingia kwenye hukumu dhidi yao
kuhusu urithi wangu, watu wangu Israeli,
kwa kuwa waliwatawanya watu wangu
miongoni mwa mataifa
na kuigawa nchi yangu. 3Wanawapigia kura watu wangu
na kuwauza wavulana ili kupata makahaba;
waliwauza wasichana
ili wapate kunywa mvinyo. 4“Sasa una nini dhidi yangu, ee Tiro na Sidoni, nanyi nchi zote za Ufilisti? Je, mnanilipiza kwa yale niliyoyafanya? Kama mnalipa, mimi nitalipiza juu ya vichwa vyenu kwa kasi na kwa haraka yale mliyoyatenda. 5Kwa kuwa mlichukua fedha na dhahabu yangu pia mkabeba hazina zangu nzuri sana mkapeleka kwenye mahekalu yenu. 6Mliwauza watu wa Yuda na Yerusalemu kwa Wayunani, ili kwamba mpate kuwapeleka mbali na nchi yao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.