Yoeli 3:19
Joel 3:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini Misri itakuwa ukiwa, Edomu itakuwa jangwa tupu, kwa sababu ya jeuri waliofanya kwa watu wa Yuda, ambao katika nchi yao walimwaga damu isiyo na hatia.
Joel 3:19 in English
Joel 3:19 · Berean Standard Bible
Egypt will become desolate, and Edom a desert wasteland, because of the violence done to the people of Judah, in whose land they shed innocent blood.
Context
17“Ndipo mtakapojua kwamba Mimi, Bwana Mungu wenu,
nakaa Sayuni, mlima wangu mtakatifu.
Yerusalemu utakuwa mtakatifu;
kamwe wageni hawatavamia tena. 18“Katika siku hiyo milima itadondosha divai mpya,
na vilima vitatiririka maziwa;
mabonde yote ya Yuda yatatiririka maji.
Chemchemi itatiririka kutoka kwenye nyumba ya Bwana
na kunywesha Bonde la Shitimu.* 19Lakini Misri itakuwa ukiwa,
Edomu itakuwa jangwa tupu,
kwa sababu ya jeuri waliofanya kwa watu wa Yuda,
ambao katika nchi yao
walimwaga damu isiyo na hatia. 20Yuda itakaliwa na watu milele
na Yerusalemu itadumu vizazi vyote. 21Hatia yao ya damu, ambayo sijasamehe,
nitasamehe.”
Bwana anakaa Sayuni!
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.